Wednesday, August 21, 2019

MAKA EDWARD MWAKALUKWA
Baada ya mpango wa kucheza soka Latvia kukwama, kiungo wa Yanga Maka Edward amejiunga na klabu ya Athletico De Tetuan inayoshiriki ligi daraja la kwanza nchini Morocco
Maka amesajiliwa na timu hiyo kwa mkataba wa miaka minne huku uongozi wa Yanga ukimpa baraka zote
Meneja wa mchezaji huyo Hussein Nyika amethibitisha mteja wake kusajiliwa huko Morocco
Mwezi Juni Maka aliwaaga Wanayanga baada ya kupata nafasi ya kufanya majaribio kwenye moja timu zinazoshiriki ligi kuu Latvia
Hata hivyo Maka hakufanikiwa kwenye mpango huo na kulazimika kurejea nchini na baadae kupata timu huko Morocco.

No comments:

Post a Comment